Wanawake katika kijiji cha Miguti, eneo bunge la Githunguri, kaunti ya Kiambu leo waliandamana kupinga ongezeko la uuzaji na matumizi ya pombe haramu na dawa za kulevya, hali wanayodai imesababisha vifo vya vijana kadhaa katika eneo hilo. Wanawake hao wanasema kuwa vijana wanne wenye umri wa kati ya miaka 19 na 35 wamefariki katika muda wa mwaka mmoja uliopita baada ya kunywa pombe hatari.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive