Wanawake wawili wasakwa kwa kuhusika na ulaghai wa M-Pesa Kisii

  • | Citizen TV
    4,366 views

    Maafisa wa usalama wameanzisha msako mkali wa wanawake wawili wanaoshtumiwa kwa kuwalaghai wafanyibiashara katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya kisii. Kisa cha hivi punde kilishuhudiwa katika eneo la keumbu ambapo wanawake hao walinaswa kwenye cctv wakiiba zaidi ya shilingi elfu tisini kutoka duka moja la mpesa. Na kama anavyotuarifu Chrispine Otieno wanawake hao wameingia mafichoni.