Wapalestina wakibeba miili ya wale waliouawa katika shambulizi la anga la Israeli huko Gaza

  • | VOA Swahili
    303 views
    Wapalestina wakiwa wamebeba miili ya wale waliouawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israeli katika Gaza, kufuatia shambulizi la kushtukiza lililofanywa na kikundi cha Kiislam cha Hamas dhidi ya Israeli Jumamosi (Oktoba 7). Maafisa wa afya wa Gaza walisema Wapalestina 198 waliuawa katika shambulizi la anga wakati mabomu yalipopiga ndani ya mji wa Gaza City, na kusambaza moshi mweusi uliotanda angani. Hamas walifanya shambulizi kubwa kabisa ndani ya Israeli lililokuwa halijawahi kutokea Jumamosi, na kuua watu zaidi ya 300 na kujeruhi mamia wengine katika shambulizi la kushtukiza lililohusisha watu wenye silaha waliovuka mpaka kuingia Israeli huku roketi kadhaa zikifyatuliwa kutoka Gaza. Shambulizi hilo liliweka historia ya uvamizi uliokuwa haujawahi kutokea ndani ya Israeli lililofanywa na idadi isiyojulikana ya wanamgambo wa Hamas wenye silaha waliovuka mpaka kutoka Ukanda wa Gaza, na kuwa pigo kubwa kwa Israeli katika mgogoro wao na Palestina tangu mashambulizi ya kujitoa mhanga ya Intifada ya Pili miongo miwili iliyopita. #israel #gaza #reels #igreels #videography #voa #hamas