Wapelelezi wahoji wahudumu wa Chiromo Braeside kufuatia kifo cha Susan Njoki

  • | Citizen TV
    1,114 views

    Maafisa wa upelelezi wanaochunguza mauaji ya Susan Njoki katika hospitali ya Chiromo, Braeside, wameanzisha msako wa mfanyikazi mmoja wa hospitali hiyo aliyetoweka baada ya njoki kupatikana akiwa amefariki. maafisa hao walipiga kambi katika hospitali hiyo leo, wakiwahoji wafanyikazi waliokuwepo wakati wa tukio hilo na wale waliomchukua kutoka nyumbani kwake. Polisi wanaamini mfanyikazi huyo anapaswa kujibu masuali. Aidha polisi pia wana kagua kanda za cctv zilizonakili dakika za mwisho za Njoki ambaye madaktari walithibitisha alinyongwa.