Skip to main content
Skip to main content

Washikadau wataka Wakenya wapande miti kumuenzi Raila

  • | Citizen TV
    250 views
    Duration: 1:25
    Mwanamazingira daktari Kalua Green ametuzwa na rais William Ruto kama shujaa kwa juhudi zake za kutunza mazingira Kati ya mamia ya wakenya waliotuzwa katika hafla ya mashujaa, daktari Kalua alipewa sifa kochokocho na kutajwa miongoni mwa mashujaa wakuu nchini kwa mradi wake wa 'plant your age', mkakati ambao unawahimiza wakenya kusherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa kupanda miche sawia na miaka yao. Kadhalika, daktari Kalua alipokea habari hizo za kutuzwa akiwa katika shughuli ya upanzi wa miti katika kanisa la CITAM Athi River, ambako aliongoza shuguli ya upanzi wa miti kumuenzi kinara wa ODM, hayati Raila Odinga. Alihimiza upanzi wa miti 80 sawia na miaka yake.