Washukiwa saba wakamatwa baada ya ufyatulianaji risasi Nakuru

  • | KBC Video
    52 views

    Polisi mjini Nakuru wamewakamata washukiwa saba na kupata bunduki aina ya AK-47 kufuatia kisa cha ufyatuaji risasi kilichosababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi na kuwaacha wengine wawili wakiuguza majeraha mabaya ya risasi. Kamishna wa Kaunti ya Nakuru Loyford Kibaara anasema afisa huyo aliuawa wakati wa makabiliano ya risasi na wahalifu waliokuwa wamejihami siku ya Jumapili katika eneo la Bondeni. Makabiliano hayo yalitokea wakati polisi walipokuwa wakilifuata genge la wahalifu wanaoaminika kuhusika na visa vya uhalifu katika eneo hilo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive