Wasichana 500 washauriwa kuhusu ndoa za mapema na dhuluma za kijinsi Nandi

  • | Citizen TV
    1,004 views

    Zaidi ya wasischa 500 kutoka maeneo mbalimbali Kaunti ya Nandi wamepokea mafunzo yanayonuia kuimarisha maadili mema miongoni mwa wasichana wadogo katika jamii. Wasichana hao vilevile walihamasishwa dhidi ya dhulma za kijinsia, ndoa za utotoni pamoja na mimba za mapema. Mafunzo hayo yalitolewa na kundi Moja la kina mama ambao wamekuwa mstari wa mbele kupiga vita ukeketaji. Wakizungumza eneo la sugut, eneo bunge la Emgwen, Viongozi wa kina mama hao walisema kuwa wasichana wengi kwa Sasa hawapati mafunzo kutoka Kwa wazazi wao kwani wanaachwa mikononi mwa walezi wengine. Kando na kupata mafunzo mbalimbali, pia walishiriki michezo mbalimbali ili kusaidia kupunguza msongo wa mawazo.