Wasichana wawili wa chifu wafuzu kwa shahada

  • | Citizen TV
    959 views

    Kampeni ya uhamasisho dhidi ya dhuluma za kijinsia imekuwa ikiangazia kuwalinda wasichana na kina mama kutokana na dhuluma kama vile ukeketaji na ndoa za utotoni. Chifu Dansen Reson wa Lokesheni ya Enoosupukia Narok Mashariki kaunti ya Narok amekuwa kielelezo cha kupigana na visa vya ukeketaji na anajivunia kuwa mabinti wake wawili wamekufuzu na kupata shahada. Susan Ndunda alitembelea familia hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.