Wasichana wengi Trans Nzoia wataabika kwa kukosa sodo

  • | Citizen TV
    250 views

    Katika kaunti ya Trans-Nzoia, wasichana hulazimika kukaa nyumbani kwa zaidi ya siku tano kila mwezi, hii ni kutokana na umaskini unaofanya wengi kukosa pesa za kununua sodo wakati wa hedhi. Shirika la Amref limeshirikiana na mashirika mengine, kuweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wanapata sodo kila mwezi, haswa katika shule zinazopatikana katika mitaa ya mabanda. Wakizungumza katika shule ya msingi ya Matisi viungani mwa mji wa kitale, wadau katika sekta ya elimu pia wamewataka wazazi kuhakikisha wanawasiliana na shule iwapo wanakabiliwa na changamoto za kupata sodo, ili kuwapa fursa ya kupata masomo bila kuhangaika.