Wataalamu wahimiza vituo vya afya ya akili Nandi

  • | Citizen TV
    152 views

    Wataalamu na viongozi wa dini kaunti ya Nandi wametoa wito kwa wizara ya afya kaunti hiyo kutilia maanani afya ya akili katika hospitali na zahanati mbalimbali .Viongozi hao wamesema kuwa kuwepo kwa idara maalum ya kushughulikia matatizo hayo kutasaidia kuimarisha huduma na matibabu ya matatizo ya akili kwani imebainika kuwa baadhi ya vituo vya afya havina wataalamu wa afya ya akili.