Watetezi wa watoto wa kike Kajiado wataka juhudi zaidi kuwekwa ili kuwalinda watoto

  • | Citizen TV
    124 views

    Wadau wa kuwatetea watoto wa kike dhidi ya dhuluma mbali mbali katika kaunti ya Kajiado wameeleza haja ya juhudi zaidi kuendelea kuwekwa ili kuwalinda watoto ambao bado ndoto yao inakatizwa. Wakizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya mtoto wa kike iliyoandaliwa Kajiado kusini, wadau hao wanasema licha ya kuwepo kwa kampeni za kuhamasisha jamii kuhusu haki za mtoto wa kike bado kuna wasichana ambao wanaendelea kudhulumiwa