Watu 10 wafariki kwenye mikasa miwili ya moto Kibra na Bomet

  • | Citizen TV
    2,814 views

    Watu kumi wamefariki kwenye mikasa miwili ya moto mtaani kibra hapa jijini Nairobi na Bomet. Katika mtaa wa Kibra, watu wanane wakiwemo mama, watoto wake wawili na kakake walifariki alfajiri baada ya moto mkubwa kuteketeza nyumba yao na kuacha makumi ya watu bila makazi. Na huko Bomet, familia moja inaomboleza kifo cha watoto wao wawili wadogo walioteketea kwenye nyumba yao.