- 113 viewsDuration: 2:45Takribani watu milioni mbili tayari wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula nchini, huku maelfu ya watoto wakiwa kwenye hatari ya ugonjwa wa utapiamlo kutokana na ukosefu wa chakula. Ripoti ya hivi punde ya hali ya chakula nchini ambayo imetolewa na shirika la kutathmini utoshelevu wa chakula (IPC) inaonyesha taifa liko katika hali mbaya na kutoa tahadhari kuwa hali hiyo huenda ikawa mbaya zaidi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa. Mary Muoki anachambua ripoti hiyo.