Watu 4 wafariki Busia baada ya kugongwa na lori

  • | Citizen TV
    3,688 views

    Watu wanne waliaga dunia Jumanne asubuhi na mwingine mmoja kupata majeraha mabaya baada ya kugongwa na lori la mchanga katika eneo la Bulemia kaunti ya Busia Akidhibitisha kisa hicho, afisa msimamizi wa eneo la Bunyala Isaaya Mose alibaini kuwa ajali hiyo ilifanyika mwendo wa saa kumi na moja asubuhi pale dereva wa lori la mchanga alipoteza mweleko, na kuwagonga watu watano waliokuwa kando ya barabara ya Port Victoria kuelekea Budalangi, wakisubiri gari la kuwasafirisha nyumbani baada ya sherehe za krismasi. Wakazi wa eneo hilo aidha walilamikia ongezeko la ajali katika eneo hilo kutokana na kile walichosema ni utepetevu wa madereva. Milli ya walioaga dunia imehifadhiwa katika makafani ya kaunti ya Port Victoria huku majeruhi akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Busia akiwa hali mahututi.