Watu 8 waaga dunia kwenye ajali ya barabarani kwenye barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi

  • | Citizen TV
    1,155 views

    Watu wanane waliaga dunia kwenye ajali ya barabarani eneo la Mlima Kiu huko Salama kwenye barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi usiku wa kuamkia leo. Na kwenye kisa tofauti, idadi ya watu waliofariki kwenye ajali katika eneo la Ikanga,Taita Taveta imefikia watu kumi na wanne baada ya watu wawili zaidi kufariki walipokuwa wakitibiwa hospitalini.