Watu kumi na mmoja wamefariki kwenye mafuriko

  • | Citizen TV
    2,604 views

    Watu kumi na mmoja wamefariki huku maelfu wakiachwa bila makao kufuatia mafuriko yaliyoshuhudiwa katika kaunti tisa nchini. Jamaa wanne walifariki Narok usiku baada ya nyumba yao kusombwa na mmonyoko wa ardhi, huku watu wawili wakifariki maji walipokuwa wakijaribu kupita kwenye daraja lililogubikwa maji Machakos. idara ya kukabili majanga imetoa tahadhari ya mafuriko katika kaunti za Tana River, Lamu na Garissa kufuatia ongezeko la maji katika mabwawa ya seven forks.