Watu milioni 4 hatarini kufa kwa Ukimwi

  • | BBC Swahili
    17,122 views
    Dunia inaweza kukumbwa na vifo milioni 4 zaidi vinavyotokana na Ukimwi kufikia mwaka 2029, kwasababu ya kukatizwa kwa misaada muhimu na Marekani. Haya ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi la UNAIDS. Ripoti hiyo pia imesema katika kipindi hicho, kunaweza kuwa na maambukizi mapya milioni 6. Hii ina maana gani kwa mataifa ya Afrika na je, yana uwezo wa kujikimu bila ufadhili huu? Kwa haya na mengine mengi, ungana na Hamida Abubakar mwendo wa saa tatu usiku katika Dira ya Dunia TV, kumbuka kutembelea ukurasa wetu wa youtube utatupata mubashara andika tu bbcswahili #bbcswahili #afya #HIV