Watu sita wamefariki kwenye ajali ya barabarani Narok

  • | Citizen TV
    1,807 views

    Watu sita wamefariki kwenye ajali ya barabarani Narok huku saba wakijeruhiwa. Ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Silanga kwenye barabara ya Narok kuelekea Mulot ilihusisha gari la aina ya Toyota Sienta lililokuwa kimetoka Mulot na lingine aina ya Subaru Forester lililokuwa likielekea Narok. Inaarifiwa kuwa gari la Subaru Forester lilikuwa likijaribu kupita gari lingine pale lilipogongana ana kwa ana na gari la pili. Watu sita walifariki papo hapo. Miili ya waliofariki imepelekwa katikamakafani ya hospiali ya rufaa ya Narok ikisubiri upasuaji.