Watu wanne katika kaunti ya Lamu watekwa nyara na walinda usalama

  • | Citizen TV
    216 views

    Wakaazi wa Wadi Ya Witu kaunti ya Lamu wamelalamikia kutekwa nyara kwa jamaa zao kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu wa kigaidi.Kulingana nao watu wanne wametekwa nyara mwezi mmoja uliopita na watu wanaoshukiwa kuwa maafisa wa usalama katika kijiji cha Witu bila maelezo yeyote kutoka kwa idara za usalama.