Watu wanne wamefikishwa mahakamani mjini Machakos kwa tuhuma za kuhusika na ulaghai wa ardhi

  • | Citizen TV
    599 views

    Watu wanne wamefikishwa mahakamani mjini Machakos kwa tuhuma za kuhusika na ulaghai wa ardhi. Wanne hao wanahusishwa na ulaghai wa ardhi ya hifadhi ya wanyamapori ya Swara, eneo la Lukenya. Wanne hao Papius Karinga Mureithi, Sebastian Sikenya, Geoffrey Moroti na Timothy Kiplagat walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Charles Ondiek japo walikosa kukiri mashtaka.