Skip to main content
Skip to main content

Watu watatu waangamia na wanne kujeruhiwa vibaya kwenye ajali eneo la Kedowa, Kericho

  • | Citizen TV
    7,432 views
    Duration: 51s
    Tunaanza na taarifa ya tanzia. Watu watatu wameaga dunia huku wengine wanne wakijeruhiwa kwenye ajali iliyotokea eneo la Kedowa kwenye barabara kuu ya Kericho kuelekea Nakuru mapema leo. Kwa mujibu wa polisi, gari aina ya toyota probox lililokuwa na abiria 7 lilikuwa linaelekea upande wa kedowa kabla ya kugongana dafrao na trela ambalo lilikuwa linaelekea upande wa Nakuru. polisi wanashuku kuwa dereva wa probox alikuwa mlevi. abiria hao walikuwa jamaa za familia moja waliokuwa wanaelekea nyumbani kwao baada ya sherehe. miili ya marehemu ilipelekwa katika makafani ya hospitali ya Londiani huku mabaki ya magari hayo yakikokotwa hadi katika kituo cha polisi cha Kericho.