Watu watatu wafariki katika ajali Tharaka Nithi

  • | Citizen TV
    446 views

    Watu watatu walifariki asubuhi kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha basi la shule ya wasichana ya Ruiri katika eneo la Njuri, kwenye barabara kuu ya Meru kuelekea Embu kaunti ya Tharaka Nithi. Basi hilo lilikuwa linawasafirisha waumini wa kanisa la Thau Methodist kutoka Tigania Magharibi kuelekea Karen, jijini Nairobi, kuhudhuria harusi. Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa dereva alishindwa kudhibiti basi hilo baada ya gurudumu kupasuka na kusababisha basi hilo kubingiria. Kamanda wa Meru kusini Eunia Onyancha amesema watu wengine wanane walijeruhiwa vibaya na wanapokea matibabu hospitalini huku wengine wakiponyoka na majeraha madogo. Basi hilo lilikuwa limebeba abiria 46