Watu watatu wameripotiwa kuambukizwa MPOX Lugari

  • | Citizen TV
    35 views

    Watu watatu wameripotiwa kuambukizwa maradhi ya Mpox katika eneo la Chekalini huko Lugari kaunti ya Kakamega. Gavana wa kaunti hiyo Fernandes Barasa amesema tayari watu hao wametengwa katika wodi moja katika hospitali ya Chekalini kwa matibabu. Basara amewataka wakazi kuwa wangalifu wanapotangamana na kujizuia kugusana ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo hatari