Watu watatu wauawa katika visa tofauti vya uhalifu Nakuru

  • | Citizen TV
    2,100 views

    Watu watatu wameuliwa katika visa tofauti vya uhalifu katika kaunti ya Nakuru katika kipindi cha siku tatu zilizopita. Paul Ndung’u, mfanyabiashara katika eneo la Ndege Ndimu eneo bunge la Bahati alipigwa risasi jana usiku, huku mwenzake ambaye pia ni mfanyabiashara katika eneo la pipeline akiuawa na majabazi kwa kupigwa risasi usiku wa jumatano. Evans asiba ametuandalia taarifa hii kwa undani.