Watu watatu wauawa na majambazi huko Chemoe Baringo kaskazini

  • | K24 Video
    37 views

    Katika shambulio jingine la ujambazi katika kaunti ya Baringo, wahalifu wenye silaha walishambulia familia iliyokuwa ikisafiri kwa pikipiki mbili kutoka marigat kuelekea Chemoe. Katika kisa cha kusikitisha, baba, mama, na mtoto wao wa miaka miwili walipigwa risasi na kuuawa katika eneo hilo la Chemoe huko Baringo kaskazini. Watu wengine watatu walijeruhiwa baada ya kupigwa risasi wakati wa shambulio hilo asubuhi.