Watu wawili zaidi wameuwawa Baringo

  • | Citizen TV
    468 views

    Watu wawili wanaoshukiwa kuwa wezi wa mifugo waliuawa siku ya Jumanne baada ya kutekeleza mashambulizi katika eneo la Longerer kaunti ya Baringo. Wawili hao walikuwa miongoni mwa wavamizi walioshambulia wakaazi usiku wa kuamkia Jumatatu, na kuiba idadi isiyojulikana ya mifugo. Viongozi wa eneo hilo wamemshutumu rais William Ruto kwa serikali yake kushindwa kudhibiti wizi wa mifugo na utovu wa usalama. Hali ambayo imesababisha familia 2700 kuhama kwao pamoja na shule 20 kufungwa.