Waumini wa kanisa la AIPCA Kayole wadai viongozi wamefuja fedha zao

  • | KBC Video
    48 views

    Mzozo umekumba kanisa la AIPCA huko Kayole, kaunti ya Nairobi ambako baadhi ya waumini wanashtumu viongozi wa kanisa hilo kwa madai ya kufuja fedha na kusalia uongozini bila ya kuandaa uchaguzi. Kundi hilo linawataka viongozi wa sasa kuondolewa na ukaguzi mpya kufanywa. Kadhalika, wamedai kuwa juhudi zao za kuwataka maafisa wa polisi kuingilia kati zimeambulia patupu huku wakitishia kufunga kanisa hilo hadi malalamishi yao yatakaposhughulikiwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive