Wawakilishi wa KMPDU wakosa kufika kwenye kikao

  • | Citizen TV
    145 views

    Kiza bado kimetanda kuhusiana na mgomo wa madaktari nchini, huku maafisa wakuu wa chama cha madaktari wakisusia mkutano uliopaniwa kutia saini mkataba wa kusitisha mgomo huo jana mchana. Kwenye mkutano na wanahabari baada ya saa za kusubiri, mawaziri na magavana waliokuwa kwenye mkutano huo wameafikia kuwapa madaktari muda hadi leo mchana kuafikia mkataba huo. Kwa mujibu wa pande zote mbili, yote yaliafikiwa kwenye mkutano wa pamoja wa Jumapili isipokuwa swala la malipo na kutumwa kwa madaktari wanafunzi. Haya yanajiri huku maafisa kliniki wakijiandaa kufanya maandamano makubwa katika barabara tofauti za jiji la Nairobi hii leo.