Wawakilishi wadi watofautiana na uongozi wa Gavana katika kaunti ya Machakos

  • | K24 Video
    112 views

    Kizaazaa kimeshuhudiwa katika mahakama ya Machakos leo mchana baada ya maafisa wa usalama wa kaunti kuvamia kikao cha mahakama na kumkamata kwa nguvu mwakilishi wadi wa Kalama Bonface Maeke. Maeke na wawakilishi wadi wenzake kadhaa ambao kwa muda sasa wamekuwa wakikosoa uongozi wa serikali ya kaunti walikuwa wamefika mahakamani kumsindikiza mwenzao Doughlas Musyoka , mwakilishi wadi wa masii. Musyoka alikamatwa jana na maafisa wa kaunti kuwa kudaiwa kufanya ujenzi wa nyumba bila kibali hitajika.