Skip to main content
Skip to main content

Wazazi Elgeyo Marakwet walalamikia gharama ya juu ya masomo

  • | Citizen TV
    89 views
    Duration: 1:18
    Huku wanafunzi wakirejea shuleni kwa muhula wa pili, wazazi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wamelalamikia kupanda kwa gharama ya maisha, hali wanayosema kuwa imekuwa kikwazo kikubwa katika maandalizi ya kurejesha watoto wao shuleni. Wazazi hao wanaitaka serikali kupunguza bei za bidhaa muhimu, hususan vifaa vya masomo kama vile vitabu na sare za shule. Wameeleza kuwa gharama ya maisha imepanda mno, jambo ambalo limewaacha wengi wao wakihangaika kukithi mahitaji yao ya kila siku.