Wazazi wa watoto walio na ugonjwa wa kupooza ubongo wakabiliwa na unyanyapaa

  • | Citizen TV
    283 views

    Unyanyapaa na uhaba wa fedha bado ni changamoto kubwa inayokabili wazazi wa watoto walio na maradhi ya kupooza ubongo, katika eneo la Yala. Wazazi hao wanasema kuwa mahitaji ya dawa kila siku na lishe maalum kwa watoto hao imewafanya wategemee msaada kutoka kwa wahisani katika mashrika ya kijamii. Wakizungumza mjini Yala katika mkutano wao wa kufunga mwaka, kina mama wanaeleza kuwa wanapitia dhiki zaidi kuishi miongoni mwa jamii na hali ya Watoto wao kwani kila mara watu huhusisha kupooza kwa ubongo na uchawi. Wanaeleza kuwa uhaba wa fedha unawalazimu kuwabeba Watoto wao kila wakati kwani gharama ya kununua kiti cha magurudumu ni ghali kwao. Mkurugenzi katika wakfu wa Omni, ambako kina mama hawa wanapata ushauri na nasaha na tiba ya mwili anasema kuna matumaini ya jamii kuelewa maradhi hayo hayatokani na uchawi au hata kusaidia katika malezi na ukuaji wa Watoto hao.