- 7,105 viewsDuration: 2:52Wazee wa jamii ya maa kaunti ya kajiado walifanya sherehe za kutabiri jinsi msimu wa mvua za vuli utakavyokuwa kaunti hiyo. Wazee hao walisoma matumbo ya mbuzi na kubaini kuwa kaunti hiyo itapokea kiwango cha chini ya wastani cha mvua msimu huo. Aidha idara ya utabiri wa hali ya anga imekubaliana na ubashiri huo kuhusu hali ya anga itakavyokuwa kwanzia mwezi oktoba hadi mwezi disemba mwaka huu.