Skip to main content
Skip to main content

WAZIRI BEATRICE ASKUL AZINDUA MRADI WA MAJI NG’ILUKIA, TURKANA MASHARIKI

  • | KNA Video
    13 views
    Duration: 1:25
    Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maendeleo ya Maeneo Kame Beatrice Askul amezindua rasmi mradi wa maji katika eneo la Ng’ilukia, Turkana Mashariki, uliotekelezwa kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Kerio Kerio Valley Development Authority. Mradi huo unalenga kuboresha upatikanaji wa maji kwa matumizi ya nyumbani na mifugo, huku zaidi ya wakazi 3,000 wakitarajiwa kunufaika moja kwa moja. Waziri Askul amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa na serikali ya kaunti katika kutekeleza miradi ya maendeleo yenye lengo la kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo kame kama Turkana.