Skip to main content
Skip to main content

WAZIRI BEATRICE ASUKUL AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI NG’ILUKIA, TURKANA MASHARIKI

  • | KNA Video
    8 views
    Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maendeleo ya Maeneo Kame, Beatrice Asukul, amezindua rasmi mradi wa maji katika eneo la Ng’ilukia, Turkana Mashariki. Mradi huo umejengwa kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Kerio (KVDA) na unalenga kuboresha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Asukul amesema wakazi wa Ng’ilukia wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji kwa matumizi ya nyumbani na mifugo. Zaidi ya wakazi 3,000 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo.