Waziri Kindiki aamrisha mifugo walioibwa kurejeshwa

  • | Citizen TV
    952 views

    Waziri wa Usalama Profesa Kithure Kindiki ametoa onyo kwa wavamizi wanaoendeleza wizi wa mifugo akiagiza mifugo walioibwa kurejeshwa mara moja kwa wamiliki. Waziri Kindiki alikuwa akizungumza katika eneo la Posta kaunti ya Laikipia alipokuwa akishuhudia zoezi la kurejeshwa kwa zaidi ya mifugo 500 walioibwa kwa wamiliki. Aidha, Waziri Kindiki ametaka ushirikiano bora kati ya wakaazi na maafisa wa usalama ili kuwakamata wezi wa mifugo