Waziri Kindiki aonya dhidi wanaopanga kuandamana

  • | Citizen TV
    8,512 views

    Waziri wa usalama Profesa Kithure Kindiki ameonya upinzani dhidi ya mipango yake ya maandamano akisisitiza kuwa serikali haitarusu mali zaidi kuharibiwa. Waziri Kindiki akizungumza alipohudhuria ibada kaunti ya Tharaka Nithi amesema serikali itakabiliana na yeyote anayevunja sheria wakati wa maandamano. Na kama Gatete Njoroge anavyoarifu, viongozi wa Kenya Kwanza pia wameonekana kumlaumu rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kile wanasema ni kusababisha mfarakano kati ya serikali na upinzani.