Waziri Kithure Kindiki asema Kenya itatumia shilingi bilioni 91 kuwatuma maafisa wa polisi Haiti

  • | Citizen TV
    636 views

    Kenya itatumia shilingi bilioni 91 katika zoezi la kuwatuma maafisa wa polisi wa kenya kulinda usalama nchini haiti. Waziri wa Usalama Kithure Kindiki amesema haya mbele ya kamati ya pamoja ya usalama bungeni ambapo pia ametoa hakikisho kuwa kuondoka kwa polisi kujiunga na vikosi Haiti hakutaathiri usalama wa Kenya. Aidha, Inspekta wa Polisi Japhet Koome pia amefika mbele ya kamati hiyo akisema ni dharura kwa polisi wa kenya kwenda nchini humo kukabiliana na ukiukaji wa haki za binaadam unaoendelea