Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry ameondoka mamlakani kufuatia uhasama

  • | Citizen TV
    225 views

    Waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry amejiuzulu kutokana na utovu wa usalama unaoendelea nchini humo. Muungano wa mataifa ya carribean unaongozwa na rais wa Guyana Irfaan Ali umethibitisha kujiuzulu kwa waziri mkuu huyo. Henry mwenye umri wa miaka sabini na nne ni daktari aliyesomea taaluma ya upasuaji wa ubongo kabla ya kushika hatamu za uongozi mwaka wa 2021 wakati rais wa taifa hilo alipouawa na wanamgambo. Henry alizuru Kenya hivi majuzi na kutia saini mkataba na rais William Ruto wa kuwezesha na kurushu kenya kutuma walinda usalama kusaidia katika juhudi za kiusalama huko Haiti. Taifa hilo limekumbwa na misukosuko huku makundi ya watu waliojihami yakitatiza shughuli za usalama.