Waziri Murkomen aahidi kuimarisha usalama bondeni Kerio

  • | Citizen TV
    1,045 views

    Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen ametaja mauaji ya kasisi Allois Cheruiyot Bett kama njama ya majangili kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya wezi wa mifugo wawili na kukamatwa kwa wengine wanne wiki tatu zilizopita katika juhudi za kukabiliana na wahuni eneo la kerio valley. Murkomen aliyefika nyumbani kwa Kasisi Bett kutoa pole zake amesema oparesheni ya kurejesha amani eneo la kerio valley itaendelea na kuongezwa nguvu kuhakikisha amani inarejea vikamilifu.