Waziri Simon Chelugui awahakikishia wakaazi wa Baringo usalama

  • | Citizen TV
    258 views

    Waziri wa biashara ndogo na vyama vya ushirika Simon Chelugui, amewahakikishia wakaazi wa Baringo kwamba serikali inashughulikia visa vya uvamizi. Hii ni baada ya polisi wa Akiba kuuwawa huko Kiserian, Baringo Kusini, alipokuwa akilinda mashine ya kuchimba iliyokuwa ikitumika Katika ujenzi wa barabara ya Kiserian-Mukutani. Akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa huko Kabarnet, Chelugui amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa wizi wa mifugo unaangamizwa Bonde la Kerio