Waziri Soipan Tuya awatembelea waathiriwa wa mafuriko Kabete

  • | Citizen TV
    516 views

    Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi, na Misitu Soipan Tuya amesema kuwa Kenya itahitajika kutafuta mbinu mpya ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Waziri huyo amesema kuwa licha ya mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi kuafikia ufadhili zaidi kutoka mataifa yanayochangia pakubwa uchafuzi wa mazingira, kiasi kikubwa cha fedha zinazoahidiwa kwa bara afrika haziwezi kusaidia kutokana na viwango vikubwa vya riba. Wakizungumza huko kabete walikowatembelea waathiriwa wa mafuriko, Mawaziri Tuya na mwenzake wa leba Florence Bore wamewaahidi waathiriwa wa mafuriko kuwa serikali inatafuta ardhi ili kuruhusu baadhi ya wahanga wa mafuriko kuhama kutoka katika maeneo ambayo yanakumbwa na mafuriko. WIzara ya afya itatoa dawa kwa waathiriwa ili kuzuia magonjwa yatokanayo na maji chafu.Zaidi ya nyumba sitini Kabate zimesombwa na mafuriko.