- 308 viewsDuration: 3:20Waziri wa elimu Julius Ogamba amewataka wahadhiri wa vyuo vikuu wanaogoma kurudi kazini akishikilia kuwa tayari serikali imechukuwa hatua na kutoa sehemu ya kiwango cha fedha kwenye akaunti zao kama walivyokubaliana. Akizungumza mjini Mombasa wakati wa kongamano la wakuu wa taasisi za elimu nchini, Ogamba pia ameonya kuwa kukiuka agizo la kuwataka kurudi kazini ni kinyume na mwelekeo wa mahakama.