Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atembelea handaki linalotumiwa na walinzi wa mipaka Ukraine

  • | VOA Swahili
    181 views
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken Atembelea handaki lililotumiwa na walinzi wa mipaka huko Kyiv Oblast na kuzungumzia uungaji mkono zaidi wa Marekani kwa Ukraine. Blinken alionyeshwa pia mavazi ya kuukinga mwili, silaha na magari ya kijeshi. Jana jumatano mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani alitangaza msaada mpya wa dola bilioni moja kwa ajili ya Ukraine. #waziri #mamboyanje #antonyblinken #ukraine #kambiyajeshi #voaswahili #voa #dunianileo #mwanadiplomasia #marekani - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.