Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen atangaza mwongozo mpya kwa polisi

  • | Citizen TV
    6,029 views

    Afisa wa Polisi hapaswi kutumia silaha dhidi ya mtu yeyote ambaye hajajihami na ambaye hana nia ya kujeruhi ama kumshambulia afisa wa usalama ama raia. Akizindua sera ya kitaifa inaYOtoa mwongozo kuhusu matumizi ya silaha katika idara ya Polisi, Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amesema utumizi wa silaha na nguvu haipaswi katika visa vya utekaji nyara, mateso na mauaji, na pia mshukiwa anapokamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha Polisi.