Skip to main content
Skip to main content

Waziri wa zamani Raphael Tuju aripotiwa kutoweka

  • | Citizen TV
    8,509 views
    Maafisa wa upelelezi wanachunguza na kumtafuta waziri wa zamani Raphael Tuju na dereva wake waliotoweka kwa njia tatanishi jana jioni. Familia ya Tuju ikisema kwamba hawajaweza kuwasiliana naye wala dereva wake Steve Mwanga. Hata hivyo, gari la Tuju lilipatikana eneo la Karen, leo asubuhi na sasa limeegeshwa katika kituo cha Polisi cha Karen.