Wenyeji wa Mahola Alego Usonga wanalalamikia wizi wa mifugo

  • | Citizen TV
    100 views

    Wenyeji wa eneo la Mahola katika eneo bunge ya Alego-Usonga wanalalamikia kukithiri kwa wizi wa mifugo katika eneo hilo baada ya zaidi ya ng’ombe 20 kuibwa katika kipindi cha chini ya siku tatu. Wakiongozwa na Mama Rose Akoth, ambaye ni mwathiriwa wa hivi punde, wakazi hao wanasema kuwa wezi wanalenga nyumba za wajane, wakilalamika kuwa licha ya kupiga ripoti kwa ofisi ya chifu na kituo cha polisi cha Mwer hakuna hatua yoyote imechukuliwa.Wajane hao wanaeleza kuwa mifugo wanaoibwa ndio kitega Uchumi chao. Kilio chao sasa ni kwa idara ya usalama kuongeza doria usiku.