Wezi wavamia makao makuu ya kampuni ya usambazaji stima (Ketraco) eneo la Kegati, Kisii

  • | Citizen TV
    1,285 views

    Maafisa wa polisi katika kaunti ya Kisii wameanzisha uchunguzi kufuatia uvamizi uliotekelezwa katika makao makuu ya kampuni ya usambazaji stima (Ketraco) eneo la Kegati ,Nyaribari Chache na kusababisha uharibifu mkubwa. Kufikia sasa kaunti yote ya Kisii imesalia kwenye giza tangu genge la majambazi kuvamia kituo hicho mwendo wa saa tisa asubuhi. Chrispine Otieno sasa anaungana nasi na maelezo zaidi.