Wimbi la makombora ya Urusi yalivyoshambulia miji ya Ukraine

  • | BBC Swahili
    4,068 views
    Urusi imefanya mashambulizi ya makombora katika miji ya Ukraine, ukiwemo mji mkuu, Kyiv. Inaonekana kuwa ndio mashambulizi yaliyosambaa zaidi tangu wiki za mwanzo za vita. Polisi wanasema takriban watu 10 wameuawa nchini humo. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la anga la Ukraine Urusi imerusha zaidi ya makombora 80 ya kulenga shabaha nchini Ukraine, huku mengi yao yakidunguliwa. #bbcswahili #urusi #ukraine