- 229 viewsDuration: 4:15Ugonjwa wa kifafa unaendelea kuwa changamoto ya afya nchini, huku maelfu ya wagonjwa wakikumbana na unyanyapaa, gharama kubwa za matibabu na changamoto ya kupata huduma za kitaalamu. Hali hiyo imechochea wito wa kuongezwa kwa uhamasisho na kuboreshwa kwa huduma za matibabu, hasa katika Kaunti ya Kajiado ambako Hospitali ya Kifafa ya AIC imezinduliwa ili kuwapa matumaini wagonjwa na familia zao.