Wizara ya afya yasitisha huduma za matibabu hospitali ya Nyanchwa kufuatia madeni ya bima ya SHA

  • | Citizen TV
    264 views

    Huduma za matibabu katika hospitali ya kanisa la Kiadvetisti ya Nyanchwa kaunti ya Kisii zimesitishwa na wizara ya afya nchini baada ya madai ya ulaghai wa mamilioni ya fedha za bima ya afya ya SHA. Aidha, barua kutoka wizara ya afya imeagiza wagonjwa wote walio kwenye hospitali hiyo kwa sasa wahamishwe hadi hospitali nyingine kwa muda wa miezi mitatu